Rozari hai


Rozari hai ni chama cha kitume ambacho hujishughulisha na kusali na kuombea ulimwengu , amabapo kimejipanga kusali rozari nzima kwa njia ya kushirikiana watu 15 , yaani kila mtu husali fungu moja na kukamilisha mafungu 15 ya furaha , uchungu , na yale ya utukufu. Hivyo basi kila mmoja anapata neema na mastahili ya rozari nzima ingawa amesali fungu moja.

Historia ya rozari hai inaanza na mt.Dominiko katika karne ya 12 , aliyepewa rozari na mama yetu na kuambiwa ilikua ni silaha na dawa ya kujiponya na wazushi hasa "Waalbijensi" na baada ya sala ya rozari takatifu wazushi hao wali ongoka na kuishi maisha ya kikristo.

Rozari hai sasa kama njia mpya ya kusali rozari hiyo aliyopewa mt.Dominiko ilianza mwaka 1826 huko Lions Ufaransa , ilanzishwa na "Paulina Marie Jaricot(1799 - 1862)".Ambaye kwa muda mrefu alikua akijiuliza , ni jinsi gani anaweza kuwafanya watu waipende rozari takatifu , kwani katika kipindi kile watu hawakupenda kabisa kusali rozari , lakini pia watu wema walikua wapweke mno , kiasi cha kuwafanya washindwe kusali , baada ya hapo Mungu alimuongoza mwenye heri Paulina Kuigawa Rozari katika Mafungu 15 na kuyagawa kwa watu 15.

Papa Gregory XVI ndiye aliyetoa idhini rasmi kuruhusu ushirika huu na kutoa rehema nyingi sana kwa watakao shiriki katika utume huu.Na tangazo rasmi kutoka kwa Papa juu ya kurusu rozari hai lilitoka 27/1/1832.

computer election
members of rozari hai

Katika seminari ya Maua utume huu ulianza rasmi tar 8 Mei 2016 ukianzishwa na ndugu Denis Budigila ambaye alifanikiwa kuanzisha kwanza kwa wafanyakazi wa Maua seminari na baadae aliweza kuanzisha kwa wanafunzi wa seminari , pia kama wanachama kutokana na maombi yao.Hivyo basi katika jumuiya yetu wapo waseminari wa Maua seminari na wana parokia ya Maua. Kipindi cha likizo waseminari hujaribu kuhamasisha juu ya ushirika huu wakiwa makwao kwa ndugu , jamaa na marafiki , ili waweze kujiunga, lakini bado hawaja fanikiwa sana , pia katika mazingira ya shule hujaribu kushirikiana na wana parokia kusali na kuwahamasisha waseminari wengine kujiunga.

Utume huu unataka kutimiza ile ahadi ya mama yetu: "Siku moja moyo wangu imakulata utaukomboa ulimwengu".Mwana chama anapaswa kuchukua kumi moja(fungu) amabyao ni wajibu wake kuisali kila siku kwani asipo fanya hivyo rozari haitokua hai tena.Pia mwanachama anaweza kuchukua makumi(mafungu zaidi) , cha msingi ni kuhakikisha anayasali yote.Pia mwanachama huvaa medali , skapulari pamoja na rozari kama silaha zake dhidi ya adui mwovu "Ibilisi".

Kama wanachama wa rozari hai seminari ya Maua , tunawaalika watu wote kujiunga na rozari hai ili kutimiza ile ayhadi ya mama yetu na kupata neema na mastahili ya rozari na kuuombea ulimwengu iwe sehemu nzuri zaidi.